An event on Football kick-off season on SuperSport held in Tanzania

Msimu wa Soka 2015/16, SuperSport inajiandaa kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.

Msimu  wa Soka 2015/16, SuperSport inajiandaa kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.

Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha  kiti chao cha Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho analenga kuhakikisha Chelsea inabaki  juu, wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.

 

Watazamaji wa SuperSport watakuwa na  nafasi ya kipekee kushuhudia mechi  kwenye ubora wa  HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya  Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga), Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya (Europa), mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia, Kombe la Ujerumani, Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la  FA na zaidi.

Katika msimu huu, Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 live, huku Wateja wa DStv Premium watazawadiwa mechi zote Live zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .

Kuanzia msimu huu na kuendelea, vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza vitakuwa vikiletwa kwenu kupitia SuperSport5 (SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium.  SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza huku ikijumuisha  mechi  3 live kila Jumamosi na Jumapili. Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum vya soka kama  PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na  Mechi za Wiki.

Moto wa La Liga utawashwa  ndani ya SuperSport3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea  mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili. Wateja wa DStv Premium na Compact Plus watapata nafasi ya kuangalia mechi za michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza, mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na Ratiba zote za Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.

Pamoja na Mechi za Live ndani ya SS3, itakuwa inakuonyesha vipindi  muhimu  vya shoo za magazeti, yanayojiri ndani ya  La Liga, pamoja na vipindi maalum  vya ligi za soka. Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa, Kombe la FA, Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la Ujerumani, Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea kutapatikana kwenye SS3 .

Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea SuperSport.

 

 

Related