Maharage gives MultChoice Tanzania donation to Al Madina

Multichoice Tanzania imefanya ziara yake kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina kilichopo Tandale.

MultiChoice Tanzania imefanya ziara yake kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo mnamo tarehe 22 Desemba. Kusudi la ziara hiyo, ilikuwa kutoa msaada msimu huu wa krismasi kwa watoto hao. Baadhi ya viongozi, wafanyakazi wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Ndugu Maharage Chande, waliwasilisha zawadi hizo kwa mlezi wa kituo hicho, aitwaye Mama Kuruthum Yussuph

 

Multichoice Tanzania ilimkabidhi mlezi wa kituo cha Al-Madina (Bi Kuruthum) vifaa mbalimbali vya kuwasaidia watoto hao katika mahitaji yao ya kila siku. Miongoni mwa zawadi zilizotolewa ni vyombo vipya vya kulia chakula, nguo, vyakula, sare za wanafunzi wa shule za msingi, vifaa mbalimbali  kwa ajili ya mahitaji ya kila siku, pamoja na kodi ya pango, Jumla ya mahitaji yote yaliyokiabidhiwa leo ikiwa ni ya Sh. Milioni tano.

 

Mnamo mwezi wa sita mwaka huu, Msimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Multichoice Tanzania ilitembelea tena kituo hiki na mojawapo ya mahitaji yaliyopelekwa ilikuwa ni Vyerehani vinne. Siku ya leo mlezi wa kituo Bi Kuruthum Yusufu ameonyesha eneo la biashara la ushonaji liloanzishwa baada ya kukabidhiwa vyerehani vile. Biashara hii inawasaidia kuwapatia kipato cha kila siku ambacho husaidia kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya watoto hawa.

 

Bi Kuruthum na watoto wa kituo cha Al-Madina walitoa shukurani zao za dhati kwa msaada uliyotolewa na Multichoice Tanzania katika kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Multichoice Tanzania imekuwa ikisaidia kituo hicho tangia mwaka 2009, mpaka sasa.

 

Akiwa anakabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Mheshimiwa Maharage Chande alisisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana na kituo hicho katika kuwawezesha watoto kusonga mbele kwani ndiyo taifa la kesho, na kila mmoja wetu ana wajibu wa kujitolea kwa namna moja au nyingine.

 

Kwa mawasiliano zaidi: Instagram (@dstvtanzania), Twitter (@dstvtz), Facebook (https://www.facebook.com/DStvTanzania/), na https://www.dstv.com