Msanii Diamond Platnumz

Kama unakumbuka 2016 nilikusogezea story ya Diamond Platnumz kutangaza kusainishwa katika label kubwa duniani Universal Music Group na leo nina good news kwako kuhusu hiyo ishu kama ni shabiki wa Platnumz.

Diamond tayari ameiachia video yake ya Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, pia Universal Music Group imetangaza rasmi kumsaini Diamond.
 
Sikiliza Marry You kwenye Mziki Fresh, Jumatano saa 18:00 kwenye Trace Mziki (323).
 
Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo na pia wimbo wake, Marry You akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music.

Maneno haya yalisikika kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Dlamini.  “Diamond ni star , msanii mwenye nguvu na kipaji kikubwa sawa na wasanii wengine wakubwa wakimataifa niliofanya nao kazi."

"Ana malengo na nia ya kufanikiwa, anajivunia nchi yake na watuwa nchi yake, lugha yake na kuitangaza viizuri tamaduni yake na napenda hicho. Diamond ni class ya kwanza katika level ya performance stegini na yupo kiafrika zaidi na hiyo itasambaa kote duniani, wasanii kama yeye ndio sababu ya sisi kufanya tunachofanya,” Sipho Dlamini alimalizia

Mengi ya Diamond na maisha yake, soma alivyopata shavu kule Afrika Kusini.