Washindi wa Harusi Ya Ndoto Yake kupitia Maisha Magic Bongo

Wakazi wawili wa jiji la Dar es Salaam ambao ni wachumba Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wameibuka washindi wa shindano la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic Bongo (160).

Wapenzi hao wameshinda zawadi ya ufadhili wa harusi yao yakifahari itakayofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi April mwaka huu. Pamoja na kushinda Harusi ya Ndoto Yao, wawili hawa pia watapewa zawadi ya fungate kwa hisani ya hoteli yakitalii ya Voyager Beach iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya.

Washindi hao walitangazwa jana katika kilele cha siku ya wapendanao katika hafla iliyofanyika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam nakuhudhuriwa na washindi hao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendajiwa MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema channel ya Maisha Magic Bongo imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi hiyo kupitia kipindi chake maarufu cha Harusi Yetu kinachorushwana channel hiyo ambacho huonyesha harusi mbalimbali.

DStv_HarusiYetu_MaishaMagicBongo_2017

Kipindi cha Harusi Yetu kilianza kuruka mnamo Novemba 2016 ambapo msimu wa pili wa kipindi hicho ulianza mwezi Julai mwaka 2017. Kipindi hicho hurusha harusi mbali mbali huku kikiangazia walikotoka wanandoa, hatua wanazopitia katika mahusiano yao na hatimaye tukio la kufunga ndoa.

Kuanzia ilipoanza awamuya pili Maisha Magic Bongo ilianzisha shindano maalum lililojulikana kama Harusi ya Ndoto Yako ambapo washiriki walikuwa wakijibu kuhusiana na kipindi cha Harusi Yetu ambapo kila wiki kulikuwa na swali moja. Hadi kufikia mwisho wa shindano mnamo mwezi Desemba mwaka jana jumla ya washiriki 1,112 walishiriki ambapo 448 waliingia kwenye mchujo wa awali na hatimaye kubakia wanne ambao waliitwa kwenye usaili maalumu lililokuwa na jopo la watahini saba.

Baada ya usaili huu, Solomon Mkaziwa Dar es Salaam pamoja na mchumba wake Magreth waliibuka washindi na hivyo kupata zawadi ya kugharimiwa harusi yao itakayofanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 28 Aprili mwaka huu.

DStv_HarusiYetu_Tanzania_2018

Akifafanua kuhusu zawadi hiyo, Maharage alisema zawadi hiyo inamaanisha maharusi hao watarajiwa watagharimiwa kila kitu kuanzia ukumbi, mavazi, chakula, vinywaji, burudani, pamoja na fungate la kukatana shoka katika moja ya hoteli za kitalii Voyager Beach Hotel katika ufukwewa Mombasa nchini Kenya.

Wakizungumza katika hafla hiyo, Solomon pamoja na mchumba wake Magreth wamesema wamefurahi sana kushinda na kutuzwa ufadhili wa harusi yao. “Sote tunafahamu ni jinsi gani zoezi la harusi linavyokuwa na patashika hususan kwenye suala la gharama. Hivyo nafurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kushinda katika shindano hili kwani sasa sisi kazi yetu ni kufikiria tu jinsi tutakavyoendesha maisha yetu kwani suala la harusi limekamilika” alisema Solomon.

Solomon pia ameipongeza Maisha Magic Bongo kwa kubuni shindano hilo ambalo lilileta msisimko mkubwa na kwamba anaamini kuwa channel hiyo itaendelea kuimarika kwani kwa sasa imekuwa maarufu sana kwa kuwa ni chaneli inayowafanya watanzania wajivunie vipaji vyao.

DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhui ya Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tasnia ya sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.

Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishwa tarehe 1 Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na sanaa hapa Tanzania na pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv. Kwa kipindi chote hiki chaneli hi iimekua kwa haraka sana ambapo kwa sasa ni miongoni mwa chaneli zenye watazamaji wengi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Chaneli hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya wasanii hapa nchini huku mamia ya wasanii wakipata fursa mbali mbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na pia kupata mafunzo na kipato kupitia sanaa.

Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa katika soko kwa sasa ni pamoja na tamthilia ya Huba,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania, pia kuna filamu na vipindi vingine kama Mwantumu, Harusi Yetu, Kitimtim pamoja na tamthilia mpya zilizoanza kuonyeshwa hivi karibuni za Sarafu na Kapuni ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.