Mchezaji wa soka Mbwana Aly Samatta

Rais Magufuli aituma pongezi yake kwa mchezaji soka Mbwana Aly Samatta

Mbwana Aly Samatta, mcheza soka maarufu wa Tanzania ambaye anaichezea club ya TP MAZEMBE ya Congo DRC alitangazwa na shirikisho la soka Afrika kuwa ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Mengi ya soka, usikose kuitazama mchuano wa La Liga kati ya Barcelona na Athletic Club, Jumapili 17 January, saa 21:30 kwenye SuperSport. Mechi hii pia unaweza kuitazama kwa Kiswahili kwenye DStv Explora yako.

Kila mmoja baada ya hapo alitoa pongezi zake kwa Samatta lakini hii ni kutoka kwa Rais Magufuli ambaye alizitoa hizo salamu na kutaka Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa Samatta.
 
Rais Magufuli amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.

Kwenye sentensi nyingine Rais amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.