launching dstv bomba

Mteja yeyote wa DStv anaweza kujiunga na kifurushi hiki kwa kulipia gharama hii, tumia njia zetu za malipo kama Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Eazy Pesa, Pay Point, Max Malipo, NMB Bank, FNB Bank, au DStv Huduma kwa wateja.

DStv Bomba ni kifurushi cha gharama nafuu, Tsh.22,000  tu kwa mwezi! Mteja yeyote wa DStv anaweza kujiunga na kifurushi hiki kwa kulipia gharama hii, tumia njia zetu za malipo kama Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Eazy Pesa, Pay Point, Max Malipo, NMB Bank, FNB Bank, au DStv Huduma kwa wateja.

Bomba ni kifurushi kinachokidhi Mahitaji ya kila Mteja, kumbuka DStv tunavifurushi vitano vyenye gharama tofauti za malipo, na Bomba ni moja kati ya vifurushi hivi. Hata katika hali ngumu ya uchumi mteja bado ananafasi ya kupata huduma zetu kwa kulipia kifurushi hiki chenye gharama nafuu, Kifurushi Bomba.

Kinakupa zaidi ya chaneli 65. Gharama ya kifurushi ni nafuu sana lakini mteja unapata kufurahia chaneli nyingi zaidi ya 65, DStv tunawajali wateja wetu na tumezingatia umuhimu wa idadi ya chaneli ili mteja aburudike na huduma zetu.

Kifurushi Bomba kinakupa burudani zote kabambe, zikiwemo za kitaifa kupitia chaneli zetu kama ITV, Star TV, Channel 10, na TBC, na burudani za Kimataifa kwenye chaneli zaidi ya 60 zilizomo baadhi yake ni Africa Magic Epic Movies, Maisha Magic Swahili , Discovery World, CBS Action, CBS Reality na CBS Drama, Select Sport 1 na 2 na nyingine kibao.

Wapenda soka na michezo hamjaachwa nyuma kwenye kifurushi Bomba, Tuna SuperSport Select na SuperSport Select 2 ambazo zitaonyesha Ligi kuu ya Uingereza, Kombe la klabu bingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Hispania, Ligi kuu ya Ujerumani, pia tuna na riadha na ngumi kwenye chaneli hizo, Bila kusahau SuperSport Blitz itawaletea habari zote za michezo.

Ukiwa na kifurushi Bomba hutopitwa na Tamthilia motomoto zinazofatiliwa na wengi mjini kwasasa, Hapa sasa ndio patamu zile chaneli zetu maarufu zaidi kwa Telenovela na Series kali masaa 24, Telemundo na Zee World zinapatikana kuanzia kifurushi hiki, kwanini sasa upitwe, usikubali kuhadithiwa tena!

Lipia kifurushi hiki ufurahie Telenovela, series za kihindi na movie kali za kihindi zinazoonyeshwa kila siku kwa Lugha ya Kingereza, bila kusahau masongi ya kihindi wale wazee wa Kuch Kuch Hotae…

Umetuelewa sasa,  DStv Bomba ni kifurushi pekee chenye mambo mengi ya kukuburudisha na kwa gharama nafuu sana, jiunge nacho leo ufurahie wewe na familia yako, na kama hujajiunga na DStv unaweza fanya hivyo sasa kwa gharama ya sh.129,000 tu, unapata vifaa vyote ikiwemo HD Dekoda, Dish pamoja na ufundi buree, kisha Lipia kifurushi cha mwezi Tsh 22,000 tu, kifurushi Bomba.