How to top up BoxOffice

BoxOffice inakuletea filamu na kukuwezesha kufanya kila kitu kupitia rimoti yako. BoxOffice inakupa mpaka filamu 21 kwa mpigo, zikiwemo filamu zilizotoka hivi karibuni kama vile kichekesho cha Trevor Noah  Welcome to America. Kodisha filamu hii kwenye BoxOffice kwenye DStv Explora yako.

Lakini kwanza unahitajika kuongeza fedha kwenye akaunti yako uweze kukodisha filamu uzipendazo. Kuongeza fedha kwenye akaunti yako ya BoxOffice ni rahisi. Chagua njia mojawapo hapa chini:

Njia ya Kwanza: Akaunti Yako- Matawi ya MultiChoice Tanzania

 • Tembelea tawi letu lolote la MultiChoice au mawakala popote pale nchini
 • Fanya malipo kama ambavyo huwa unafanya kwa kujisajili kwenye vifurushi vya DStv
 • Kumbuka tu kuweka wazi kwamba unalipia kwa ajili ya kukodisha filamu kupitia BoxOffice

Njia ya Pili: Lipia Kama Inavyoelekezwa Hapa Chini

 • Kupitia huduma ya Selcom USSD na kupitia vituo vya malipo zaidi ya 10,000 vilivyopo nchi nzima.
 • Vituo vya kulipia vya MaxMalipo nchi nzima.

Njia ya Tatu: Akaunti Yako - AIRTEL

 • Piga/Andika *150 *60# kuingia kwenye menyu ya Airtel Money
 • Chagua 2. Chagua Biashara/kampuni au 3. Ingiza jina la biashara/kampuni (300000)
 • Chagua 1. Kujiunga TV(Subscriptions)
 • Chagua 5 Box Office
 • Ingiza Kiwango cha Pesa
 • Ingiza Namba ya Kumbukumbu ( namba ya mteja au kadi)
 • Ingiza namba yako ya siri(PIN) ya Airtel Money

Njia Ya Nne: VODACOM

 • Piga/Andika *150*00# kuingia kwenye menyu ya Vodacom M-PESA
 • Chagua 4. LIPA kwa M-pesa
 • Chagua 3. Chagua kwenye orodha or 4. Weka namba ya kampuni
 • Chagua  1. Kingamuzi
 • Chagua 1. DStv
 • Chagua 2. BoxOffice
 • Ingiza Kiwango Cha Pesa
 • Ingiza namba yako au namba ya kadi.
 • Ingiza namba yako ya siri(PIN) ya M-PESA

Njia ya Tano: TIGOPESA

 • Dial *150*01# to go to Tigopesa menu
 • Piga/Andika *150*01# kuingia kwenye menyu ya TigoPesa
 • Chagua 4. Kulipia Bili
 • Chagua 2. Kupata jina la kampuni/biashara
 • Chagua 5. Kujiunga TV (TV Subscriptions)
 • Kisha 6. DStv BoxOffice
 • Chagua 1. Namba ya Kumbukumbu ( namba ya mteja au kadi)
 • Ingiza kiwango cha pesa
 • Ingiza namba yako ya siri(PIN) ya TigoPesa