Msanii wa bongo Dully Sykes

Dully Sykes aongea na DStv kuhusu jina la Simba na ni nani aliyeimiliki.

Jina la Simba limechukua headlines za mwanzomwanzo mwaka 2016 baada ya Mr. Blue kusema anafurahi kuona huwa anaanzisha vitu alafu watu wanaiga akimtolea mfano Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni amekua akitumia Simba kama a.k.a.

Mkongwe wa bongofleva Dully Sykes amekaa kwenye exclusive na DStv.com na kusema, "Mr Blue na Diamond ni wadogo zangu wananiheshimu sana na ninawapenda sana, siwezi kuongea sana kuhusu hii ishu ila wale ni wadogo."
 
Mbali na jina hiyo ya Simba, kutana na wasanii hawa wakimenyana kwenye charts za Mzooka Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Akaendelea: "Wangapi walishaanza kujiita Simba? Najua Mark 2B Simba Marehemu ndio alikua akijiita hivyo, Afande Sele akajiita Simba dume ila jina Simba lenyewe ni la Mark 2B, sio mbaya Mr Blue akijiita Simba na Diamond akijiita Simba, basi na mimi nitajiita Sungura."
 
Dully ameongeza kwa kusema: "Ni jina ambalo mtu unajiita tu, sioni sababu ya kugombana kwa kitu ambacho hakina faida yoyote, kweli sioni sababu ya kugombania hilo jina."
 
Kwa kumalizia, Dully Sykes amesema huwa nikiona wanagombana hivyo siwezi kuwapigia simu, wale wameshakua wakubwa..... utagombania vipi jina la mtu la Mark 2B? acha wote wawe Simba tu... wanagombania nini sasa? Hilo ni jina ambalo halina chochote.
 
Usikose kuitazama Mzooka na mengine mengi kwenye Maisha Magic Bongo. Kumbuka haya yote unaweza kurekodi, kuchezesha tena (rewind) na pia kusimamisha wakati wowote (pause) kwenye DStv Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:
 
Fill out my online form.