Ben Pol na Jux

Kwenye exclusive, Ben Pol asema walitoa wimbo Nakuchana baada ya comments ya mashabiki

Mwimbaji staa wa R&B Tanzania Ben Pol amesema wimbo wake mpya na Jux Nakuchana ni wimbo ambao waliuandika pamoja baada ya kuona kelele za mashabiki.

Ben amesema kuna vitu vingi wamekua wakiviona kwenye comments za mashabiki na ndio maana kila mmoja akamchana mwenzake kwenye huo wimbo japo haimaanishi kwamba vilivyoimbwa ndani vina ukweli.
 
Jux naye amesema ilibidi wautoe huo wimbo baada ya kuona umeshavuja mtaani na mashabiki wamepata copy ya wimbo ambao haujamaliziwa vizuri.
 
Kitendo cha wawili hawa kwenda Arusha na kuona mashabiki wanataka waimbe huo wimbo mpya kiliwafanya waone hii ni hit song sababu imeanza kuombwa na mashabiki hata kabla haijatoka.
 
Kwenye moja ya mistari ambayo Ben amemchana Jux, ni pamoja na ishu ya kulelewa na Vanessa Mdee... unaweza kuusikiliza wimbo kamili kwenye Clouds TV (294).
 
Pia unaweza rekodi single hii na hits zingine kwenye DStv Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi: 
 
Fill out my online form.