Clouds TV logo

Clouds TV imeingia rasmi kwenye king'amuzi cha DStv Chaneli 294

MultiChoice tunapenda kuwatangazia wateja wetu  na Watanzania kwa ujumla kuwa Clouds TV sasa imeingia rasmi kwenye DStv Chaneli 294.

Kile kilio cha muda mrefu cha watazamaji na wapenzi wa Clouds TV juu ya kukosekana kwenye king'amuzi cha DStv kimesikika na sasa Clouds TV imeingia rasmi ndani ya DStv.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja  Uendeshaji  MultiChoice Tanzania  Ndugu Ronald Baraka Shelukindo, amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Clouds TV na DStv, MultiChoice na Clouds wamefikia muafaka ambapo watazamaji na wapenzi wa Clouds TV wenye ving'amuzi vya DStv watapata uhondo wa Clouds TV na wa DStv.

Akiongezea, Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania, Ndugu Salum Salum ameelezea furaha ya kampuni yao na akasema,  wakati mwingine walikuwa wanashindwa kufikia lengo la kupata wateja wengi zaidi kutokana na kukosekana kwa Clouds TV hivyo kuanzia sasa, tunaimani kuwa idadi ya wateja itaongezeka maradufu!.

Clouds TV itaanza kupatikana rasmi ndani ya DStv tarehe 14 Januari, kwenye Chaneli 294, katika vifurushi  vyake vyote ikiwemo; Premium, Compact Plus, Compact , Family na kifurushi cha Bomba.

Kwa picha clear ya HD, pata Clouds TV kwenye DStv Explora yako na pia uweze kurekodi na kuchezesha tena vipindi uvipendavyo (rewind). Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:

 

Fill out my online form.