NFS launch in Tanzania

Mechi zote 760 za misimu mipya ya Ligi Kuu Ya Soka Uingereza (Premier League) & Ligi Kuu Ya Soka Hispania (La Liga) zitapatikana kupitia DStv

  • Mechi zote 760 za misimu mipya ya Ligi Kuu Ya Soka Uingereza (Premier League) & Ligi Kuu Ya Soka Hispania (La Liga) zitapatikana kupitia DStv
  • SuperSport itawaletea watazamaji na wapenzi wa soka michezo kabambe ya soka kuliko ambavyo imewahi kuonekana kabla kutoka kwenye UEFA Super Cup, Ligi Ya Mabingwa ya UEFA, Kombe la FA, Kombe la Capital One, Super Cup ya Hispania, Fainali ya Copa Del Rey, German Cup na mingine mingi.

Msimu mpya ya Ligi bora za soka ulimwenguni imewadia na kuanzia Jumamosi tarehe 13 Agosti, Ulimwengu wa Mabingwa, SuperSport, utawaletea mashabiki wa soka barani Afrika michuano yote moja kwa moja (Live) ya msimu mpya katika kiwango cha HD kupitia DStv!

Mashabiki wa soka mlipatiwa kionjo cha msimu ujao wa soka mwishoni mwa wiki iliyopita wakati DStv ilipoonyesha pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu la kugombea Ngao Ya Hisani ambalo lilishuhudia Man United wakitwaa kikombe cha kwanza mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu Ya Uingereza msimu uliopita, Leicester City. Na kama shauku na mpagao wa msimu uliopita ni dalili ya chochote, basi msimu huu mpya wa Ligi Kuu Ya Soka Uingereza utakuwa sio wa kawaida huku mechi zote 380 zikipatikana kupitia DStv.

Kwa uhakika mechi zisizopungua 300 zitaonyeshwa moja kwa moja kitu ambacho kinathibitisha kwamba SuperSport ndio mpango mzima kwa wapenzi na watazamaji wa soka na matukio mengine ya kimichezo barani Afrika. Chaneli hii ya michezo hukuletea matangazo kwa mapana na marefu ambayo hujumuisha uchambuzi wa kina wa Premier League kutoka kwa wachambuzi mahiri wa soka ambao hawana upinzani kokote barani Afrika.

Msimu huu unaokuja utaleta kivutio kikubwa zaidi huku Premier League ikiwa na mechi za siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza. Hizi pia zitakuwa sehemu ya ofa kutoka SuperSport kwenda kwa mashabiki wa soka. Kama kawaida siku za Jumamosi zitaendelea kuwa za soka kwa mechi zinazoanza saa Kumi Jioni (4pm) kwa saa za Afrika ya Kati ambapo SuperSport itakuwa inarusha hadi michezo mitatu ya ziada kwa wakati mmoja kupitia chaneli mbalimbali za SuperSport SS3, SS5, SS6, SS7 na SS11. Chaneli maarufu ya Premier League ya masaa 24 itaendelea kuwepo kupitia SS11 kuendelea kuthibitisha kwamba SuperSport ndio makazi ya soka la kimataifa.

Kwa wapenzi wa soka la Ligi Kuu ya Uingereza, patakuwa na burudani mfululizo na bila kuchelewa kwani pia kutakuwa na wiki tano ndani ya msimu ambapo kutakuwa na michezo ya katikati ya wiki ambayo itarushwa  katika siku za Jumanne na Jumatano.

Msimu unaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti na kumalizika 21 Mei, 2017.
 

Lakini Sio Hayo Tu!!

Wateja wa kifurushi cha DStv Compact wataendelea kufurahia soka kutoka katika ligi kabambe ulimwenguni. SS11 itaendelea kuwa makazi maalum ya Ligi Kuu Ya Uingereza huku SuperSport 12 ikiwa tena chaneli maalumu ya masaa 24 kwa ajili ya Ligi Kuu Ya Hispania (La Liga) ambapo timu kama Real Madrid na Barcelona zitakuwa na mengi ya kuvutia pindi msimu mpya utakapoanza tarehe 19 Agosti 2016.

Shukrani kwa muda tofauti wa kuanza kwa mechi za La Liga, asilimia 80% ya mechi 380 zitaonyeshwa Live. Mechi zilizobakia zitaonyeshwa kwenye SS5 au SS7 aidha Live au kwa kuchelewa.

Ligi ya Europa (The Europa League) pia itaonyeshwa kwa matangazo ya mechi zote 205 huku mechi 120 kati ya hizo zikionyeshwa moja kwa moja(Live). Michuano mingine kabambe itakayoonyeshwa kupitia SuperSport ni pamoja na FA Cup, Capital ONE Cup, Spanish Super Cup, Copa Del Rey final na German Cup.

Ili kuhakikisha kwamba wapenzi wa soka wa DStv hawatokosa tukio lolote, kutakuwa na matangazo kutoka pande zote za dunia kupitia tovuti ya SuperSport na pia app mpya ya SuperSport, zote ambazo zitakuwa na live streaming na pia video za yaliyojiri na kuvutia wengi. Huduma maarufu ya DStv Catch Up iliyopo kwenye DStv Explora pia itakuwa na matukio yaliyojiri kutoka kwenye mechi zote kubwa.

Kupata Explora yako kwa urahisi, jaza fomu hii:

 

Isitoshe, matokeo ya mechi zinazoendelea, matokeo na habari za papo kwa hapo zinaweza kupatikana kupitia tovuti ya supersport.com, app na simu au vifaa vingine vya viganjani (mobile versions).

Kwa taarifa zaidi kuhusu soka ambalo halipatikani kwingine kokote zaidi ya DStv na mechi zinazokuja na mengi mengineyo tafadhali tembelea SuperSport.