BET WINNER, MTV, WINNER, Tanzania'S  SINGER

Baba mzazi wa mwimbaji Diamond Platnumz alihojiwa na D'wikend Chat Chow ya CloudsTV na kuongea mengi ambayo Watanzania hawakuwahi kuyafahamu.

 
Baba amesema "Nimekuwa shabiki sana wa Diamond na moja ya nyimbo zake unazozikubali kutoka kwake ni Nitarejea, imenipa fundisho sana, sio peke yangu haswa nyimbo zake zote anaandika vizuri ila hii imenigusa sana".
 
Kuongelea fundisho, je umepatana na Mariam wa Migomba akiongelea utamaduni wa Uswahilini na masuala ya familia? Tazama Mchikicho wa Pwani, Jumamosi saa 23:30 katika katika Maisha Magic Bongo (160)
 
 Akiendelea kumuongelea mwanae  alizidi kusema "Namwambia afunge mkanda Mwenyenzi Mungu atamsaidia, kuna mambo mengi yamewahi kuandikwa kwenye magazeti na yakanichukiza, wanamkandia sana mwanangu, hizi ni fitna tu... kilichoniudhi zaidi ni pale wanaposema Diamond hanisaidii". -Baba Diamond
 
Abdul anasema "Hata hivyo mimi simlazimishi Diamond kuninunulia chochote manake pia hata mimi nina uwezo wangu kiasi ila inanikasirisha sana waandishi kuandika magazetini kwamba hanijali".
 
Kwa kumalizia, Baba mzazi wa Diamond anasema "Mara ya mwisho kuonana na mwanae huyo ilikua ni kipindi alichomvisha Wema Sepetu pete ya uchumba. pamoja na hayo amekua akinitumia pesa za matunzo".
 
Mbali ya Mchikocho wa Pwani, unaweza kuitazama DStv Catch Up ambayo kuna filamu za kimapenzi mwezi huu wa Februari kwenye DStv Explora. Jaza fomu hii kupata Explora yako kwa urahisi:
 
Fill out my online form.