Msanii wa Tanzania Alikiba

Alikiba Kutangazwa kuperform ndani ya One Musical Festival London

Hii ndio list nimekusogezea ya wasanii wa Afrika waliochaguliwa kupanda stage za One Music Festival jijini London, Ungereza 13 May 2017 na Alikiba kama msanii kutoka Tanzania aliyechaguliwa.

Alikiba, Cassper Nyovest na Olamide wametangazwa kuwa miongoni mwa wasanii wa Afrika watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.

Uliyaskia ya Vanessa Mdee na dili yake mpya Nigeria? Twakuletea yote hapa.

Kwa sasa ungana na Alikiba kwenye Bongo 10 kila Alhamisi saa 20:00 ndani ya TRACE Mziki (323).

One Music Festival wameandika kwenye akaunti yao ya Instagram: “Msanii mpya kabisa kutambulishwa kutoka Tanzania @officialalikiba atakaye burudisha wadada wa SSE Arena, Wembley London 13 May."

Lakini bado wasanii wengine wawili watatangazwa wiki hii.
 
Alikiba anakuwa msanii wa tatu kutoka Tanzania kuwahi kutumbuiza kwenye tamasha hilo. Diamond na Vanessa Mdee walitumbuiza kwenye matamasha yaliyofanyika nchini Marekani katika awamu tofauti.