Mtanzania Wema Sepetu

Staa na mrembo  kutoka kwenye soko la filamu Tanzania bongomovie Wema Sepetu amerudi tena upya kwenye movie baada ya kukaa kimya kwa muda kwenye masuala hayo.

Wema Sepetu ambaye wengine wanamuita Kamanda kama ambayo wanaitwa wanachama wa Chadema abacho Wema amehamia baada ya kutokea CCM.

Wema akishirikiana na muigizaji Gabo Zigamba wamekuja na filamu fupi inayoitwa Kisogo ambayo imepokelewa vizuri sana na baadhi ya walioweza kuitazama mara baada ya kuzinduliwa rasmi mwezii huu.

Tazama bongomovie ya Limbukeni siku ya Ijumaa kuanzia saa 17:30 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).

Filamu hiyo inahusisha masuala ya ushirikina na wasichana wa kazi (wafanyakazi wa ndani) wanavyojihusisha na ushirikina kwenye kutusaidia majumbani. Watu wamesifia uhalisia wa filamu hiyo na namna ambavyo wachezaji wameweza kufikisha maana halisi.

Pia pata uhondo chungu nzima ndani ya Huba kwenye Maisha Magic Bongo, soma mengi hapa.

Movie hiyo imepata maoni mazuri na kutabiriwa kufanya vizuri hata nje ya Tanzania.

Naye Gabo Zigamba amesema, "Wema anajua sana kuigiza, na ana uwezo mkubwa sana ila kuna wakati anakuwa haonekani kwenye movie kwa sababu ni mtu mmoja anachagua sana kazi za kuwepo na kutokuwepo. Mimi na Wema tumefanya jitihada zetu kuhakikisha ile dhana ya kuwa Bongomovie imekufa Ifutike."

Soma mengi kuhusu hofu aliyonayo Idris Sultan kipindi hiki cha Ramadhan.