Profesa Jay rasmi bungeni

DStv yaongea na Mbunge rasmi wa Mikumi Morogoro Profesa Jay ambaye kitambo alikuwa msanii wa bongofleva

Ni miongoni mwa mastaa wachache waliozichukua headlines za kutoka kwenye bongofleva, kuingia kwenye siasa na kufanikiwa kushinda uchaguzi vile vile.

Joseph Haule ndio jina lake la kuzaliwa lakini Watanzania walimfahamu sana kwa jina la 'Profesa Jay' na sasa ni mbunge wa Mikumi Morogoro kwa tiketi ya CHADEMA.

Kutana na watu wengine mashuhuri, wajasiriamali, viongozi wa jamii na siasa, kujadili mada mbalimbali kuanzia utamaduni wa kiuchumi ya Tanzania kwenye Mboni Jumamosi saa 15:00 EAT kwenye Maisha Magic Bongo.

Yafuatayo ni mambo aliyoyaongea na dstv.com kwenye exclusive interview hapa Dodoma ambapo cha kwanza ni kuwataja baadhi ya Wabunge aliokua akiwakubali.

Marehemu Deo Filikunjombe aliyekua Mbunge wa Ludewa Njombe, ni miongoni mwa waliokua wakimvutia Prof, anasema: "Sio kwa sababu ni marehemu ndio nimemtaja ila kiukweli Deo alikua jembe, alikua CCM lakini hakusita kuikosoa."

Mwingine alietajwa na Profesa Jay ni Mbunge Easter Bulaya ambaye alikua CCM lakini kwa sasa yuko CHADEMA, Prof. alisema, "Spirit ya watu kama hawa ndio imekua ikinijenga kimawazo zaidi na kuvutiwa na mengi wayafanyayo.... nimemkubali Easter toka akiwa CCM, ni jembe."

Profesa Jay amesema amekua Mbunge hata kabla hajaingia bungeni sababu nyimbo zake zimekua zikitetea wananchi toka enzi hizo lakini sasa kapewa rungu lenyewe, kinachofata ni utekelezaji tu.