Huba Cast on MMB

Mambo moto moto kwenye Msimu mpya wa HUBA , Imerudi ikiwa na mambo matamu zaidi!

Tunazungumzia  wale waigizaji wako mahiri kutoka bongo movie na bila kusahau imeongeza sura mpya za mastaa wakubwa kwenye tasnia yetu. Nadhani unawafahamu  Bi Mwenda, Ramie Ganis, Grace Mapunda, Muhogo Mchungu na Auntie Ezekiel.

Basi soma na ujue Huba msimu huu umetuandalia nini na sababu kubwa ya wewe uvutiwe kuitazama kila siku kuanzia siku ya Jumanne tarehe 13 Juni saa 19:30 Usiku hapo Maisha Magic Bongo (160).

DEV

Dev Fuli ni jina langu kijana msomi, mstaarabu, mneyekevu, na nina mwenye kujituma katika kazi zangu. Pia natambulika kwa misimamo wangu haswa kwenye maswala ya mapenzi kwa Tima. Mapenzi yetu yalistawi japo haikuwa kazi rahisi kutokana na historia iliopo katika familia zetu.  Msimamo wangu huo ndio chanzo kikuu cha mifarakano kati mimi na mama yangu mzazi Tesa. Mama yangu alalazimisha nimuoe Batuli lakini haikufanikiwa.

Na katika msimu huu bado mahusiano yangu na Tima yana sua sua na ni baada ya mama yake kukataa kabisa kushindwa safari hii akamletea Jojo.  Binti mrembo sana wenye historia nae hapo nyuma, nikajikuta  bado naendela kupambana na matakwa ya mama yangu, mbali na hayo Dev na Tima wanabarikiwa kupata mtoto na changamoto kati yao bado zinakuwa nyingi sana mmoja ikiwemo Jojo na kingine ni Clay mwanaume atakayefanikiwa kuuteka moyo wa Tima.

 

TIMA

 

Tima Kashaulo- Mimi mtoto wa Mgeni na Kashaulo ni msichana ambaye nimezaliwa katika familia ya kimaskini na sikuweza  kupata nafasi ya kusoma pia ni naweza kusema sikuwa najitambua lakini ni shupavu na mwerevu nisiyekubali kupelekeshwa ovyo ovyo, pia napishana kauli mara kw mara na mama yangu Mgeni haswa pale mama alipogundua nina mahusiano na Dev na cha kushangaza kama kuna kitu mama yangu na Tesa walikubaliana ilikuwa ni kuhusu mimi na Dev Walipambana lakini hakuna aliyefanikiwa.

Lakini katika msimu huu mpya mahusiano yetu yalianza vizuri tu na baraka ya mtoto juu 

CLAY

Mimi Clay ni mwanaume mtanashati marudai sana  mwenye mambo mengi sana. Nikisema mambo mengi, namanisha wanawake. Katika season hii nafanikiwa kukutana na Tima katika kipindi kibaya sana katika maisha yake kwani alikuwa na augomvi na mpenzi wake Dev. Mimi nakuja kuingilia na kufanikiwa kumteka Tima, kwa kifupi Clay anakuja kuleta kitim timu kati yao wote na ndiyo season hii.

JOJO

Mimi ni Jojo, mwanamke rijali mashalaah kabisa ambaye nilikuwa na mahusiano na Dev kipindi cha nyuma akiwa masomoni ulaya.  Sasa nimerudi tena na nataka kuwa na mahusiano na Dev tena ila hakuna anaye jua hili lakini  mamake Dev, Tesa ndiye aliyenituma kuvuruga mahusiano ya Tima na Dev. Kwa ukweli ntafanikiwa hapa na pale na baadae kugundua mambo mengi sana kuhusu familia ya kina Dev na Tesa na hapo ndipo uhondo unapo noga zaidi katika season 2. Itabidi umetazana Maisha Magic Bongo(160) kupata uhondo!