Ben Pol during an interview wit the DStv Mic

Mkali wa RnB Tanzania Ben Pol ametaja moja ya vitu ambavyo vitabadilika kwake ikiwemo gharama za kufanya nae colabo moja 2017

Mkali wa RnB Tanzania si mwingine bali Ben Pol ambae anafanya vizuri kwenye game na ni miongoni mwa wasanii ambao jina lao limekuwa zaidi kwa mwaka 2016.

Ben Pol ametaja moja ya vitu ambavyo vitabadilika kwake ikiwemo gharama za kufanya nae colabo moja 2017 ambapo ameieleza wazi kwenye ukurasa wake wa Twitter.

“Kuelekea 2017 bei yangu ya Collabo itakuwa $5000. So kama una project na mimi tuwasiliane before 31st Dec 2016,” Ben ameandika kwenye twitter yake.

Patana naye mwimbaji huyu na video zake kali kwenye TRACE Mziki, channel 323.

Baada ya kumpata kwenye exclusive intreview aliongea haya: “Ni kweli, ila kama wimbo ni mkali tunaweza kukaa mezani na huyo mtu akanipa sehemu ya umiliki wa hiyo kazi. Kwanza nataka kupunguza idadi ya colabo ili nifanye chache za walio serious na wanaoweza kupush hizo project. Mfano mtu hawezi kukulipa dola elfu 5 halafu akaiweka ngoma kwenye album, au akaiweka ndani tu.” 

“Pia itasaidia kwangu kufikiria zaidi kwenye hiyo kazi, hakuna mtu atakulipa dola 5 halafu akatarajia disappointment, so ita-benefit kwa pande zote.”