Diamond Platnumz na mama yake

Mama Diamond aongea kwenye exclusive kuhusu babake Diamond

Mama mzazi wa mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platinumz amesema hatopenda kuendelea kuona magazeti au mitandao inaandika kuhusu Diamond kutomjali baba yake mzazi.

Ameamua kusema haya sababu ameendelea kuona vyombo vya habari vikiendelea kuandika hizo habari wakati ukweli ni kwamba hakuna hata kimoja chenye ukweli.

Mbali na mamake Diamond, kutana na Diamond Platnumz mwenyewe akikuletea nyimbo zake kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Namnukuu akisema:, "Diamond kila mwezi anamtumia baba yake pesa ya kula, mimi ni shahidi.... wananikera sana wanaosema hamtunzi baba yake, wanajuaje?"

Mama Naseeb kaendelea: "'Mnataka kulazimisha tupige picha kuonyesha ushahidi au? Mimi sipendi kabisa wanaoleta hizo habari, Diamond hana tatizo na baba yake na anamtunza kila mwezi."

Diamond alishawahi kukiri kutokua na uhusiano mzuri na baba yake mzazi miaka iliyopita lakini sasa hivi anasema hakuna tatizo na alimsamehe kwa kumtelekeza na kutomsaidia kwenye maisha.

"Nilikua na hasira nae lakini mwisho wa siku nikaja kuona ni mzazi wangu na siwezi kumnunia, nikamsamehe maisha yakaendelea na huwa tunawasiliana," alisema Diamond.