Diamond Platnumz

Ni haya ndio yaliyoendelea kwenye MAMAs 2015

Jumamosi, 18 July ndio zilizotolewa tuzo za MAMAs (MTV Mama Awards 2015) kwenye jiji la Durban South Africa zikiwatunuku wasanii mbalimbali wa Afrika kwa kazi nzuri waliyoifanya mwaka uliopita.

Tanzania ilikua ikiwakilishwa na Diamond Platnumz na Vanessa Mdee kwenye tuzo hizo ambapo wengine kutoka Afrika Mashariki walikua Sauti Sol wa Kenya, Jose Chameleone na Bebe Cool wa Uganda.

Usiwe na shaka, kama hukupatana na wasanii hawa, jiunge nasi kwenye MAMAs 2015 Jumanne alhasiri 21 July saa 19:45 kwenye MTV Base (322).

Ukihitaji kuona ilivyokua kuanzia kwenye red carpet na mpaka ndani kwenye ushindi uliopatikana tazama picha hapa chini manake ripota wako wa DStv.com Millard Ayo alikuwepo mwanzo hadi mwisho kwenye tukio.

 

 

 

Usikose kumtaza Diamond akipokea tuzo la Best Live kwenye MAMAs 2015 Jumanne 21 July saa 19:45 kwenye MTV Base (322).