Msanii Dogo Janja

Msanii wa bongo Doggo Janja kazawadiwa gari na Madee.

Msanii wa Tiptop Connection Dogo Janja ambaye yuko chini ya usimamizi wa Madee amejikuta kwenye furaha kubwa baada ya kuzawadiwa gari na Madee.

Ungana na Jeremy Clarkson, Richard Hammond and James May kwenye show ya magari ya Top Gear kwenye BBC Brit (channel 120).

Ilikua ni suprise Madee kaifanya japo hakuwepo eneo la tukio wakati Janja anakabidhiwa hili gari ambapo baadae ilibidi Janja aandike 'shukrani sana mshua uko mbali lakini umenisuprise, sina cha kukulipa zaidi ya kukuheshimu Daima'
 
Kwenye sentensi nyingine Dogo Janja aliandika, 'Sasa hivi barabarani tunapigiana honi tu, shukrani sana Mungu akuweke'
 
Dogo Janja ametajwa kuwa na nidhamu toka aliposamehewa na kurudishwa chini ya usimamizi wa Madee.
 
Madee ni mtu wa headlines za magari ambapo amekua akinunua gari binafsi la kutembelea kila anapotoa wimbo mpya.