Christian Bella na Koffi Olomide

Mengi kuhusu Christian Bella na Koffi Olomide kurekodi single pamoja

Kwenye headlines kubwa kwenye burudani mwaka 2015 Tanzania, hii ya kolabo ya Christian Bella na Koffi Olomide haiwezi kukosa namba za juu kabisa.

Kupata hii single tu itakapotoka, endelea kuitazama kipindi cha muziki cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Haikuwa rahisi kwa Bella kutimiza ndoto zake za kufanya kolabo na Koffi aliyetamani kufanya naye kazi toka akiwa mdogo lakini hatimaye ndoto ikatimia zaidi ya wiki tatu zilizopita.

King Dodo ambaye ndio amehusika toka na kuwasiliana na Koffi Olomide, ameongea kwenye exclusive na dstv.com na kuweka wazi jinsi ilivyokua na kufichua kumbe Koffi Olomide alikuwa anakijua kipaji cha Christian Bella toka miaka hiyo.

Kumbe kaka yake Bella aliwahi kufanya kazi kwenye band ya Koffi Olomide miaka hiyo, na Koffi mwenyewe aliwahi kumwajiri Bella kama mwimbaji kwenye band yake lakini Bella akachomoa.

King Dodoo ameiambia dstv.com kwamba hata juzi walipokua pamoja studio, Koffi alikumbushia mpango wake wa kumuweka Bella kwenye band yake na kusema anatamani bado siku moja itokee Bella ajiunge nae kwenye timu ya ushindi.

Koffi na Bella wamesharekodi audio yao na sasa kinachosubiriwa ni video ambayo Koffi Olomide amekubali pia kuifanya na imependekezwa ikafanyike Dubai.