Rapper Young Killer

Rapper wa bongofleva Young Killer amezungumza na DStv kuhusu picha yake aliyoipost akiwa na askari.

Rapper kutoka bongoflevani Young Killer ameizungumzia ishu ya picha yake aliyoipost kupitia Instagram akiwa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania.

 Kuna taarifa ambazo zilitoka mwanzoni kwamba Killer kakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi lakini yeye amezikanusha na kueleza chanzo cha yote.

Nunua Explora yako leo, upate habari za mastaa wengine kwenye kipindi cha Wendy Williams Show Jumatano saa 22:00 kwenye BET (129).

Amesema akiwa kwenye safari yake kanda ya ziwa na marafiki kwenye gari walisimamishwa na askari wa usalama barabarani kutokana na gari lao kuzidisha mwendo na sio kwa kosa jingine zaidi ya hilo.

Baada ya kusimamishwa waliomba msamaha kwa kosa hilo na wakati wakizungumza na Askari, askari hao waligundua kwamba kuna Young Killer ndani ya gari ambae kumbe huwa wanasikiliza nyimbo zake, wakasalimiana kwa furaha na Young Killer ndio akaomba kupiga nao picha na kuipost.

Young Killer amesema walisamehewa kosa lao na akaipost ile picha akiwa na hao askari kama kuwashukuru pia kwa kushabikia muziki wake.