Rapper wa Tanzania Young D

Young D afafanua mengi zaidi kuhusu kolabo na Patoranking.

Kama umekua mfuatiliaji wa page mbili za hawa mastaa basi utakua umekutana na vitu tu vya kukustua kwamba wanafanana kimuonekano.
 
Baada ya kufananishwa kwa muda na hata mashabiki kucomment kwa wingi kwenye page zao za Instagram, rapper kutoka Dar es Salaam Young D amethibitisha mpango wa kazi ya pamoja.
 
Anachosema ni kwamba tayari wameshakubaliana kufanya kolabo na Patoranking ambaye ni staa kutokea Nigeria akiwa na hit single 'My Woman' ambayo ni number 1 kwenye CloudsFM Top 20 sasa hivi.
 
Ungana na wasanii kama Patoranking kwenye kipindi cha Official Naija Top 10 kila Jumatano saa 20:05 kwenye MTV Base.
 
D amesema hata juzi Diamond alipokwenda kufanya show kwenye tamasha la MultiChoice Content Showcase Mauritius, Pato aliulizia kuhusu Young D kwahiyo inaonyesha hata yeye mwenyewe amevutiwa kufanya kolabo na Mtanzania huyu.
 
Young D ameongezea namba kwenye list ya mastaa wa bongofleva na headlines za kolabo na wakali wa Nigeria akiwemo Nay wa Mitego, Diamond, Shetta na V Money