Yamoto band wakiwasiliana na Diamond Platnumz Afrika Kusini

Pata kujua ni kwa nini Diamond na Yamoto waonekana Afrika Kusini pamoja.

Band bora ya muziki kwenye bongofleva kwa mujibu wa tuzo za KTMA 2015, Yamoto ipo Afrika Kusini kwa ajili ya kukamilisha moja ya ndoto zao kubwa kwenye muziki.

Diamond ameamua kuweka mikono yake ili kufanikisha utengenezaji wa video mpya ya Yamoto chini ya Director God Father ambaye amefanya video nyingi ikiwemo za Davido, Diamond na mastaa wengine.

Ungana na Diamond na mastaa wengini mjini Durban, kwenye tuzo la muziki la MAMA 2015, itakayopeperushwa Jumamosi 18 July kwenye MTV Base.

Kwenye post yake Diamond baada ya kuweka hii picha ameandika:

Mudaa huu hapa Joburg na @i_am_godfather tukipanga namna ya utaratibu mzima wa Video ya@Yamoto_Band utavyokuwa Kesho.. OYA! #ChezaKwaMadoido.

Video hii itakua ya kwanza kwa Yamoto kuifanya nje ya Tanzania tena na director mkubwa wa muziki Afrika na inatarajiwa kuchezwa hata kwenye vituo vikubwa vya kimataifa ikiwemo TRACE Urban (DStv Channel 325), MTV Base (322) na kwengine.