Ommy Dimpoz

Msanii Ommy Dimpoz aongea na DStv na kueleza anavyojiandaa kwa tuzo la AFRIMMA.

Mwimbaji wa bongofleva Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wakali wa bongofleva watakaomiliki stage ya tuzo za AFRIMMA 2015 huko Dallas Texas Marekani.

Kwenye exclusive na dstv.com, Ommy amesema amejiandaa vizuri na kitu kingine kikubwa ni kwamba ataperform na dancer wake ambao anasafiri nao kutoka Tanzania.

Kuungana na wasanii wengine wa bongo, usikose kuitazama kipindi cha Mkasi TV unayoletewa na Salama Jabir, kila Jumapili saa 19:00 kwenye Maisha Magic East.

Ommy ambaye hatotoa single mpya mpaka uchaguzi mkuu wa Tanzania umalizike, amesema anajua AFRIMMA na nafasi aliyopata sio ndogo hivyo amekomaa ili afanye vizuri siku hiyo.
 
Tuzo za Afrimma ni tuzo zinazozidi kusogea juu kwa ukubwa na huwa zinatolewa nchini Marekani ambapo mastaa mbalimbali wa Afrika huwa wanahusishwa kama vile 2Face, Davido, Fally Ipupa, Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee na wengine wengi.
 
Tuzo za mwaka huu zinatolewa October 10 2015 ambapo wataokuwa wakihost ni wachekeshaji Kansiime wa Uganda na Basketmouth wa Nigeria.