Msanii Harmorapa kutoka Tanzania

Harmorapa ni kijana Mtanzania aliyepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii katika kipindi kifupi kwa kile alichodai kuwa watu wanamfananisha na Harmonize msanii kutoka kwenye label ya WCB ya Diamond Platnumz.
 
 
Harmorapa anafanya mziki wa rap, akiwa na nyimbo mbili mpaka sasa. Japokuwa watu wamekuwa wakiongelea sana mambo anayoyafanya nje ya muziki wake ikiwemo kuwepo kwenye matukio mbalimbali ambayo watu hawakutegemea kumuona.
 
Kutana na Harmorapa kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Harmorapa amekuwa akijitokeza, mfano tukio kama la Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuzungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza baada ya kuondolewa uwazir, kusababisha watu kumuita Harmorapa mzee wa kiki kwa matendo ambayo amekuwa akifanya.
 
Kama jina la Harmorapa ndio unalisikia kwa sasa ni kijana ambaye game ya bongofleva ilimpokea alipotoa single yake ya kwanza ya Sitoi Pasi. Hamorapa sasa hivi ameachia kazi nyingine inayoitwa Harmorapa Kiboko ya Mabisho aliyomshirikisha mkongwe Juma Nature.

Kwa kifupi Harmorapa amekuwa midomoni mwa watu kila siku na hata anapoona watu hawamuongelei basi atafanya tukio lolote ili apate kuwepo kwenye midomo ya watu