Christian Bella na Koffi Olomide

Msanii wa Tanzania Christian Bella adakua ilivyokuwa kufanya kolabo na msanii maarufu Koffi Olomide

Mwimbaji staa wa muziki wa dance Tanzania Christian Bella amezimiliki headlines time hii baada ya kuingia studio kurekodi kolabo na Koffi Olomide wa Congo DRC, staa ambaye amekua akitamani kufanya nae kazi toka akiwa mdogo.

Ukiendelea kungoja kolabo hii, pia unaweza kuburudika na single zingine za Bella kwenye kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Ilikua ni ndoto ya Bella kama ilivyo ndoto kwa vijana wengi wa Congo ambao wamekua wakimuona Koffi kama mfano wa kuigwa kwenye muziki Afrika.

Bella anasema ilifikia time akajua labda Koffi Olomide asingekubali kufanya kolabo naye sababu ya ukubwa alionao Koffi, lakini Mungu akaweka green light na Koffi akakubali ikabidi Bella apande ndege haraka kwenda Congo DRC.

Wamesharekodi single yenyewe ila bado video tu, na Bella anasema sehemu ya kipisi maarufu kwenye single mpya ya Koffi ya Selfie kimerudiwa kwa kuongezewa uzuri kwenye hii single mpya.

Kingine alichokipenda Bella ni kwamba Koffi pamoja na ukubwa wa jina lake haringi hata kidogo, studio yenyewe alikua anamuuliza Bella: "Vipi hapo nimeimba vizuri au nirekebishe?"

Furaha aliyo nayo Bella haikuachwa juu juu bali Koffi alimualika kwenda kwenye birthday party ya Cindy, mrembo ambaye amekua kwenye band ya Koffi kwa kitambo tu, hapo pia walipata nafasi ya kuzungumza mengi mazuri.