Please upgrade your browser. An upgraded browser will make your computer safer, and improve your web experience.

DStv.com works best in the latest versions of Internet Explorer,Firefox, or Chrome,

Not now

Jackline Wolper na Harmonize

Tunafahamu couples ziliotrend na kuleta gumzo kubwa kwa mwaka 2016, moja wapo ikiwa hii ya mrembo muigizaji wa bongo movie Jackline Wolper na msanii kutoka WCB Harmonize.

 
Licha ya wawili hawa kuwa katika penzi nzito na kushindwa hata kujizuia ambapo walikuwa wakionesha mahaba hadharani kusemekana kuachana baada ya Jackline kupost kuachana na Harmonize na kuifuta post hiyo iliokuwa na picha ya Harmonize.
 
Jackline ameandika maneno ambayo yameonesha kuumizwa sana kwenye penzi hilo na Harmonize mpaka kuamua kuweka wazi kupitia post hiyo.
 
Maneno alioyaandika Wolper na kufuta kwenye instagram page yake ni haya: "Nina akili timamu me siyo mtoto mdogo, endelea na maisha yako its over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.”
 
Baada ya post hiyo ya Jackline kufutwa, Harmonize akaamua kupost picha yenye caption na kuandika maneno akiashiria kuwa ameachwa kupitia maneno haya: 
 
''Haiba vepe........??? @soudybrown mwanaume akiachwa chunguza vizuri kabila lake mana sio kwa umakonde huu nilio zaliwa nao "
 
Mbali na ishu ya mapenzi, kutana na msanii huyu Harmonize na hit yake ya Matatizo kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.