ex wake diamond platnumz. Sema kutupa mbao!

Mwigizaji Wema Sepetu baada ya headlines za muda mrefu za uigizaji, ameingia kwenye headlines nyingine nzito baada ya kuthibitisha kwamba anagombea Ubunge.

Post hii ni maalum kwa Miss Tanzania wa 2006 ambaye kiki zake zimekua za muda mrefu toka avishwe taji hilo.

Mwigizaji Wema Sepetu baada ya headlines za muda mrefu za uigizaji, ameingia kwenye headlines nyingine nzito baada ya kuthibitisha kwamba anagombea Ubunge.

Kwenye kauli zake hii ni mojawapo "Nimethubutu na sitorudi Nyuma.... Niko tayari kwa mashambulizi ya aina yoyote, Wanawake tunaweza!"

Kwenye sehemu pia ya hashtag zake Instagram Wema ameandika "Wanawake tunaweza, Wanawake na maendeleo, ajira kwa vijana, kidumu chama cha mapinduzi na Tanzania katika muonekano mpya."

Wema pia kwenye sentensi zake amekiri kwamba baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu ni miongoni mwa waliomshawishi sana aingie kwenye siasa. "Nakumbukaga my late daddy Sepetu alishawahi kuniambia kuwa nijaribu kujiingiza katika politics since yeye na siasa ilikuwa ni kama uji na mgonjwa... and I remember nilimwambia ,Daddy Sepetu  no sitoweza".

Wema anasema kwamba babake alikuwa heart broken sana maana alihisi aikijaribu ataweza hii maneno ya siasa. Haswa kilichokuja kumvunja moyo ni  wema ailipochukua uamuzi wa kufanya International Business na sio hata Political science au chochote kilichohusu siasa chuoni. But hakukata tamaa... Akazidi kumwambia anweza naye ailizidi kukataa...

Wema aliendelea akiandika "Daddy Sepetu wangu, this is for you.... Leo hii nimejikuta mwenyewe nimefanya uamuzi mzito wa kujiingiza kwenye siasa na kuona wat it has in store for me".

Twamtakia kila la heri Wema kwenye juhudi zake za kisiasa.

Lakini hivi sasa endelea kupokea filamu zingine za Kiswahili kila siku kwenye Maisha Magic East. Patana na siasa za I Think I Hate My Wife Tuesday, 23 June saa 20:00 CAT.