Mtanzania Wema Sepetu

Mrembo na muigizai kutoka Tanzania, Wema Sepetu kama ambavyo wamembatiza jina la Tanzanian Sweetheart ameona sio vibaya kuwajulisha watu kuwa hana tatizo kabisa na wanaomsema kuhusu shepu yake kuwa ni fake.
 
Ni muda sasa maneno yamekuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema anajiongeza nguo ndani (kigodoro) ili kufanya aonekane mwenye shepu nzuri. Wengine wakaongeza kuwa ametumia madawa ya kujiongeza umbo na baadaye yamemkataa na kufanya shepu yake kuwa mbaya.
 
Wema amekuwa akiyasikia maneno hayo na ameamua kusema kuwa ndiyo alivyoumbwa na hakuna wakubadilisha hivyo.
Ameandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa Instagram, "Shepu ya mwendokasi ndo niliojaliwa nayo. Kama imeanzia kiunoni kwenda magotini ndo niliojaliwa nayo. Kama wewe hauna basi mshukuru Allah, ndo nilivyoumbwa jamani."
 
Kutana pia na mwanadada mwingine ambaye kwa mara nyingi ameulizwa kuhusu shepu yake Kim Kardashian kwenye kipindi cha Keeping Up with the Kardashians ndani ya E! Entertainment (124), siku ya Ijumaa saa 21:55.
 
Aliongezea, "Sio mimi bali ni Maulana ndo alionibariki nayo. Hata ingekuwa kwanzia kichwa hadi vidole vya miguuni ni sawa pia ndo niliojaliwa nayo."
 
Wema Sepetu alimalizia, "Sometimes najiangalia kwenye kioo sijimalizi. Ndo majaliwa yangu na ndo yangu basi. Sio shepu ya kawaida, niacheni na shepu yangu jamani. Siwezi kuitoa."