BBA 2014 winner Idriss and Wema Sepetu

Wema Sepetu aongea na DStv kuhusu Idris na bodyguard.

Ninao mastaa wawili wa Tanzania sasa hivi ambao ni mwigizaji Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan.

Kwenye exlucusive interview na dstv.com Wema amekanusha kuhusu stori kwamba yuko mapenzini na Idris baada ya kuanza kupost picha zake na yeye kwenye mitandao.

Nunua Explora yako leo, upate habari za mastaa wengine kwa clear picha ya High Definition kwenye Wendy Williams Show Jumatano saa 22:00 kwenye BET (129).

Wema anasema Idris ni mshikaji wake sana tu kama walivyo marafiki wengine na zaidi pia wameonekana kwenye video moja ya bongofleva ambayo ni Wanjera ya Ommy Dimpoz.

Kuhusu bodyguard, Wema amesema huwa anatembea na mlinzi wa kiume lakini sio wakati wote, anakwenda naye kwenye matukio makubwa makubwa tu sababu ya wingi wa mashabiki.

Anasema siku za kawaida hawezi kutembea naye, pia kuna kipindi chupa zilishawahi rushwa kwake baada ya mashabiki kukasirika pale ambapo bodyguard aliwazuia kupiga naye picha.

Hata hivyo Wema anasema hata ukimuona na mlinzi haimaanishi kwamba hawezi kuongea na wewe, anaweza na hata kupiga naye picha inategemea mazingira tu.