Mwigizaji Wema Sepetu

Wema Sepetu afafanua mengi kuhusu Aunty Ezekiel

Mwigizaji Wema Sepetu amezungumza kwa mara ya kwanza toka baby shower ya Aunty Ezekiel kufanyika na yeye kushindwa kuhudhuria.

Kama unakumbuka, Aunty alihojiwa na kusema pamoja na urafiki wao mkubwa, Wema Sepetu alishindwa kuenda kwenye baby shower labda kwa sababu alikua ametingwa na mambo mengi.

Ungana na waigizaji wengine kutoka bongowood kwenye filamu ya Miss Detective, Friday 12 June saa 22:30 kwenye Maisha Magic East (158).

Kwenye Interview na Wema Sepetu, amesema haya, "Nilishindwa kwenda sababu ya vitu flani flani hivi vilitokea ambavyo sipendi kuviongelea sasa hivi.

Tumeshakaa tukaongea tukayamaliza, bado sijakwenda kumuona mtoto wa Aunty sababu sijapata time ila soon tu nitafanya hivyo." Wema Sepetu.

Hata hivyo kudhihirisha kwamba yeye na Aunty hawana beef, Wema amepost picha za Aunty kwenye Instagram page yake.

 

Related