Msanii wa Tanzania Lavalava

Label ya WCB ya Diamond Platnumz imeongeza member mpya Leo May 22

 
Label ya WCB ya Diamond Platnumz imeongeza member mpya. Msanii huyo anaitwa Lavalava na atakuwa anafikisha idadi ya wasanii watano ambao wapo chini ya label hiyo.
 
Lavalava anasema alikuwa chini ya WCB tangu mwaka 2015 kwa ajili ya kuangaliwa kama anafaa kusajiliwa na katika muda huo ilishawahi kupita mwaka mzima hakuonana na Diamond hali ambayo ilikuwa inampa wasiwasi na uoga wa kutokuwa na uhakika kama amepokelewa vizuri. 
 
Kutana na Lavalava kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160).
 
Lavalava amesema, "Kuna watu walikuwa wananisifia naweza ila Diamond hakuniambiaga, nakumbuka nimewahi kukaa mwaka mzima sijaonana naye na tupo ofisi moja. Nilishasota sana na muziki ila nikasema hapa nitakaa tu nisubirie rizki yangu."
 
Amemalizia, "Ngoma yangu mpya inaitwa Tuachane ipo Wasafi.com lakini pia video ipo tayari na itakuwa kwenye YouTube muda sio mrefu naomba tu support ya mashabiki, kijana wenu ndo nimeanza nina imani kubwa ninyi ndo mnaweza kunifikisha mbali."