Msanii wa bongofleva Dogo Janja

Msanii wa bongofleva Dogo Janja amekaa kwenye exclusive Interview na reporter wa DStv Tanzania Millard Ayo na kueleza vitu angependa kuviona vinatokea kwake mwaka 2016.

Dogo Janja ambaye sasa hivi ana new single inaitwa My Life amesema kuna vichwa viwili tu anatamani kufanya navyo kolabo Tanzania kwa wakati huu ambapo mmoja ana-rap na mwingine anaimba.
 
Kolabo zingine za wanabongo unaweza kuzitazama kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).
 
Janjaro amesema, "Mtu wa kwanza ninatamani sana kufanya nae kolabo mwaka huu ni Diamond Platnumz, yaani Diamond hata akipiga mruzi kwenye wimbo wangu mimi nitafurahi.... hata asiimbe, apige tu mruzi iandikwe featuring Diamond pale."
 
Kuhusu kuongea na Diamond na jinsi ya kupiga nae hiyo kolabo, Janjaro amesema bado hajaongea nae lakini anaamini hilo litafanyiwa kazi na uongozi wake ili kufanikisha.
 
Janjaro amemtaja msanii mwingine anaetaka kupiga nae kolabo kuwa ni Madee ambaye ni kama mzazi wake, anasema angependa kurekodi kolabo ya kuchana mwanzo mwisho na Madee.