Msanii Ray C

Mwimbaji hodari wa kitambo kwenye bongofleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amehojiwa na DStv.com na kueleza kidogo kuhusu kuwa na familia.

Ray C ambaye hivi karibuni ameonyesha jitihada za kujinasua kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, amesema anapenda sana watoto lakini hayuko tayari kuzaa au hata kuwa na boyfriend kwa sasa.
 
Kutana na Ray C kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
"Nilipokua na tatizo kwenye dawa za kulevya nilipoteza relationship yangu mwenyewe, sikuwa na relationship na Rehema, sikuwa na relationship na Ray C kwa hiyo sasa hivi naiona thamani yangu, inabidi niwe mchoyo wa thamani yangu kwa sasa."
 
Ray C amesema pia kwamba ni kweli alijaribu kujiua mara nyingi lakini Mungu ndio alitaka awe hai mpaka leo. "Uwepo wangu duniani mpaka leo ni kuwapa nguvu pia waliokosa tumaini, nimepitia mengi mpaka leo na ninasema lile lilikua pepo."
 
Ray C ameyasema hayo akiwa kwenye media tour ya kuitangaza zaidi ngoma yake mpya inaitwa Unanimaliza ambayo tayari imesambazwa kwenye mitandao na kwenye radio, video yake inatoka ndani ya wiki tatu kutoka sasa.