Watanzania kwenye Hipipo Awards 2017

List ya watanzania walijizolea Tuzo za Hiphipo Uganda

Tunafahamu jinsi gani inapendeza na kuona fahari pale wasanii wa nchi yako kupata tuzo nje ya nchi hii inaonesha namna muziki unakuwa kwa kasi. Good news hii nakuletea.

Hipipo ni tuzo zilizofanyika huko nchini Uganda na watanzania wakiwemo kwenye ving'anyiro kadhaa kuwania tuzo hizo ambapo Jumamosi ndio zilitolewa tuzo na watanzania wa watatu kujizolea tuzo hizo nyumbani.
 
Usiku wa tuzo hizo ambapo pia wasanii Navykenzo waliperfom kwa stage ila pia ni miongoni mwa wasanii waliopata tuzo hizo wakiambatana na Diamond Platnumz mwenye Tuzo mbili pamoja na Alikiba.
 
Kutana na Navy Kenzo kwenye Mziki Fresh, Jumatano saa 18:00 kwenye Trace Mziki (323).
 
Hizi ndizo tuzo na category walizochukua wasanii hawa wa bongofleva all the way from 255.
 
Quinquennial Africa Music Vanguard Award – Diamond Platnumz
East Africa Best VideoSalome by Diamond Platnumz ft Ray Vanny
Song of the Year Kenya Unconditionally Bae by Sauti Sol & Alikiba
Song of the Year Tanzania Aje by Alikiba
East Africa Best New Act – Navy Kenzo