Wastara aongelea huzuni ya kubomolewa nyumba zake kwenye interview na DStv

Tunamjua mwigizaji Wastara ambaye movie zake tuliziona sana kwenye Maisha Magic Bongo ya DStv, ni mwigizaji wa Tanzania ambaye umaarufu wake uliongezeka akiwa kwenye ndoa na mwigizaji marehemu Sajuki.

Alichonacho leo kwenye DStv kupitia ripota Millard Ayo ni kuhusu kubomolewa kwa nyumba zake mbili zilizopo Tabata Dar es Salaam ambapo serikali inasema zipo kwenye bonde la Mto Msimbazi na Wananchi hawatakiwi kuishi humo.
 
Kutana na waigizaji wengine wa Tanzania kwenye bongo movie Crazy Desire, Jumamosi saa 19:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Wastara amehuzunika sababu anasema serikali ndio ilikosea tangu siku nyingi kupanga mji na sasa Wananchi wameshahamia na kuweka makazi ndio nyumba zinabomolewa.
 
Nyumba hizi mbili zake tayari zimeshapigwa X na iwapo zitabomolewa itakua ni hasara ya zaidi ya milioni 108 ambazo alijikusanyia kidogokidogo kwa kuokoteza mpaka akamaliza kujenga, nyumba yake ya pili ndio kwanza juzi ameiweka umeme, bado ni mpya.
 
Wastara amesema anahuzunishwa maana sasa hivi yeye na ndugu zake wanaishi bila amani sababu hawajui wataishi vipi baada ya hapo na hana nyumba nyingine, ni kurudi kwenye maisha ya kupanga nyumba tena.