Msanii wa Tanzania Ommy Dimpoz

Mkali wa longtime kwenye game ya bongoflevani kutoka Tanzania, Ommy Dimpoz anaefanya vizuri kwenye game na ngoma yake mpya aliyoipa title ya Kajiandae featuring Alikiba.

Kutana na Ommy Dimpoz kwenye kipindi cha mziki cha Mzooka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Katika mahojiano mafupi na msanii Ommy Dimpoz kilichomake headlines na kikamfanya aingie kwenye post ya leo kikubwa alichokizungumza ni kuhusu wasanii wengine kununua viewers YouTube.
 
Msanii huyu amesema, "Mimi nataka kutoa wito maana siku hizi watu 'wanachiti' sana hususan kwenye mambo ya views Youtube. Mimi ningewaambia kitu kimoja fanya ngoma kali video acha watu waangalie."
 
"Kwa sababu naongea kwa uzoefu wangu mimi na video yangu ‘Wanjera’ ilikuwa na views laki tisa, kuna mtu mmoja akaniambia siwezi kumsema ni nani ila aliniambia bwana vipi unataka views YouTube? Nikamuuliza views YouTube kivipi, akaniambia hebu nitumie link ya video yako. 
 
So mimi nilikuwa nataka kuprove nikamtumia link ya 'Wanjera' na ilikuwa na views laki tisa na elfu nne hivi lakini baada ya kumtumia masaa sita baadae akaniambia angalia kuangalia nakuta na milioni moja,” alifafanua zaidi.