Siwema na Nay wa Mitego

Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili huko Mwanza.

Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na chombo cha habari kilichoripoti ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili ila vyombo vya habari viliripoti kwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.
 
Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv kupitia ripota wa Tanzania Millard Ayo na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.
 
Mengi kuhusu mastaa wa bongo na maisha yao, basi itazama show ya Inside Bongowood, kila Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Amesema kilichompeleka Siwema jela ni kumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.
 
Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.