Msanii kutoka Tanzania Bushoke

DStv.com inae msanii mkongwe kutoka bongoflevani Bushoke kwenye exclusive ambaye ameelezea juu ya mipango yake ya mbeleni kimaisha ndani na nje ya fani ya muziki.

Msanii Bushoke ambae amerudi tena baada ya kimya kirefu ameachia hit single ya Mpita Njia hivi karibuni chini ya label yake Bushbox Production ambayo inamilikiwa na baba yake mzazi na leo ametueleza juu ya ndoto zake anazotaka kufikia kimaisha.

Burudika na hii ngoma mpya ya Bushoka kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.

Bushoke amesema, "Kikubwa kabisa source yangu mimi ukiacha mbali na mziki napenda niitwe mkulima au mfugaji na naona kama ntakua successful katika hivi hii itakuwa ndoto yangu kubwa sana."

Bushoke pia ameongelea kuwa alikuwa na plan ya kufanya muziki tu since day one lakini ukija kwa swala lingine kimaisha unatakiwa uwe na plan B lakini zaidi ametaja ndoto yake nyingine ambayo anataka kufikia ndani ya mziki.

Msanii huyu ameendelea kusema, "Of course kwenye muziki ninafikiria kuwa na studio yangu na kama ambavyo tuna studio South Afrika na tuna kampuni kwa hiyo ni kusema tu lini itakuwa kubwa na itaweza kumanange watu lakini ndoto yangu kubwa ni kama niliyotaja awali agriculture iko ndani yangu."