Internet ilichafuka Tanzania baada ya Wasanii wawili bongoflevani Vanessa Mdee na Shilole kurushiana maneno kupitia account zao za mitandao ya kijamii.

Haijajulikana bado chanzo hasa ni nini lakini maneno yalitoka kwenye pande hizo mbili ambapo hata hivyo post hizo zilifutwa baadae. Mengi kuhusu mastaa wa bongo na maisha yao, basi itazama show ya Inside Bongowood, kila Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo
 
Kwenye moja ya post Vanessa Mdee aliandika "Nikupe kikii ujulikane au sio? kila siku twanyamaza ndio mtugaragaze, mimi sio wale uliowazoea."
 
Shilole naye aliandika "Vee jipange mwenzio wa Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori nimekuja na mbio za Mwenge."
 
Wawili hawa walitafutwa na DStv.com na hawakuonyesha dalili zozote za kupatana kwani V alisema 'Nimeshasema kila kitu ambacho kinahitaji kusemwa kama umesoma post yangu, sihitaji kurudia kitu."
 
Shilole alisema "Acha nimnyooshe kapanic. kuona say my name imetoka na mimi kuzinguliwa sitaki, kuna mahali kaenda kuniongelea vibaya na asitamani kuonana na Shishi."
 
Hayo ndio maneno ya Wawili hawa walipohojiwa na DStv.com na hawajataka kuongea zaidi ila tungependa kuona wanapatana na amani inarejea, kila mmoja ana mchango wake kwenye bongofleva.