Msanii Vanessa Mdee kutoka Tanzania

Baada ya kutoa single yake mpya kali ya Cash Madame, Vanessa Mdee sasa ametangaza ujio wa album yake kama album yakwanza tangu aingie kwenye game ya bongofleva ambayo ameipa jina la Money Mondays.

Zaidi ametaja siku ambayo ataachia album hiyo ambapo ni March 2017 pia aliongezea haya.
 
“It’s a good time for me, it’s my first album and I am excited, ninamwachia Mungu inshallah kila kitu kitaenda sawa,” 
 
Album hiyo itakuwa na collabo kibao za kimataifa na pia kushirikisha watayarishaji mbalimbali barani Afrika.
 
Sote twaingoja hii album ya Vee Money, lakini kwa sasa kutana burudika na hit yake Cash Madame kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.