Msanii Mtanzania Vanessa Mdee

Mimi kama ripota wako wa DStv Tanzania Millard Ayo, swali nilimouliza mwimbaji wa bongofleva Vanessa Mdee anavyoona muziki wa bongo bila kiki unatembea kwa sasa?

Kwa burudani tele, ungana na Vanessa kupitia kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Jibu lake ni, "Mimi sio mpenzi wa kiki na kwa muda mrefu sana sijafanya chochote ambacho ni kutafuta kiki, huwa nafanya muziki tu lakini watu hawajui hata ni gari gani naendesha."
 
"Ni jinsi tu ambavyo industry ilivyo hata kwa wenzetu vitu vipo na wanatengeneza kiki kwa kiasi flani wenyewe kuna heshima ya usanii wanaipata na sio heshima tunayoielewa mimi na wewe, wengine wanakodisha magari na nyumba ili waonekane so ni 50 kwa 50."
 
"Kuna watu wanahitaji kiki duniani kwa sababu hawana sanaa sana ndio maana inabidi watengeneze kiki ili wauze, kuna ambao hawana kiki lakini ni wakali na wako juu mfano Adele ni msanii ambaye hata jina la mtoto wake silijui lakini akisimama akaimba kila mtu anasisimka, hivyo ni mtu na mtu."
 
Akaongezea, "Kuna wasanii wengine kabisa wametoboa na wanashika nafasi za juu lakini hawana kiki, wale ambao wanaona hawana sanaa sana ndio wanatengeneza kiki ili kubaki kwenye vichwa vya habari."