Vanessa Mdee kutoka Tanzania

Miongoni mwa wasanii waliopata mafanikio na wanaoendelea kutoboa huwezi kuacha kumtaja Vanessa Mdee, mwanadada anayefanya vizuri sasa hivi na anayehit na song yake Cash Madame pamoja na Juu akimshirikisha mpenzi wake Juma Jux.

Kutana na Vanessa Mdee na hit yake ya Cash Madame kwenye Mziki Fresh, Jumatano saa 18:00 kwenye Trace Mziki (323).

Hitmaker huyo wa Cash Madame amefanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wachache ambao watasikika katika mixtape ya watayarishaji wa muziki wa Nigeria ambao wanafanya kazi zao nchini Uingereza, Legendury Beatz.
 
Vanessa Mdee pia atafanya collabo na rapper Tay Grin kutoka Malawi. Yote yasome hapa.
 
Mixtape hiyo imepewa jina la Legendury Beatz na kupitia mtandao wao wa Instagram, wathibitisha hilo kwa kuandika:
 
“Of course the sexy @vanessamdee all the way from Tanzania, came through saucin on the #Afropop101 certainly certified!!!  #LegenduryBeatz.”
 
Wasanii wengine watakaosikika katika mixtape hiyo ni pamoja na Mr Eazi, Simi, Niniola, Timaya na Wizkid (wote kutoka Nigeria) na R2Bees (Ghana).