Msanii kutoka Tanzania Vanessa Mdee

Mdada kutoka bongoflevani anaefanya vizuri kwenye game ya mziki kwa Afrika Mashariki Vanessa Mdee kutoka Tanzania ambae tunae kwenye DStv.com leo ni mmiliki wa hit song ya Niroge.

 
Sote tunamfahamu Vanessa kama mwanamuziki lakini leo nakufahamisha kuwa pia ni mwandishi mzuri wa nyimbo na miongoni mwa wasanii aliowandikia nyimbo ukijumuisha na za kwake binafsi ni wasanii kutoka South Afrika Mafikizolo.
 
Kama mmoja wa wagombeaji wa tuzo la MAMAs 2016, kutana na Vanessa Mdee kwenye MTV Africa Music Awards itapeperushwa moja kwa moja siku ya Jumamosi 22 Oktoba saa 21:00 CAT kwenye MTV Base (322).
 
Vanessa alielezea jinsi ilivyotokea mpaka akaandika nyimbo hiyo. "Ilikuwa ndoto yangu kufanya kazi na Mafikizolo. Sikutegemea kabisa kuandika wimbo wa Mafikizolo ambao watautoa kama wimbo wao mpya uitwao Kucheza.
 
Vanessa alimalizia, "Pili ningependa kumshukuru Dj Maphorisa kwani alinipa mawazo tofauti tofauti kipindi tulipokuwa studio baadae Mafikizolo wakaukubali kwa hiyo nitahusika kama mtunzi kwenye wimbo wao mpya."