Msanii kutoka Tanzania Baraka the Prince

Nisamehe ya Baraka the Prince ambayo ni collabo yake na Alikiba ni kati ya ngoma ambazo zinafanya vizuri kwenye industry ya bongofleva Tanzania.

Burudika na single hii ya Nisamehe kwenye show ya Bongo 10 kila Ijumaa saa 20:00 ndani ya Trace Mziki (323).

Baraka the Prince ameamua kufunguka ya moyoni kwa kutoa comment baada ya beef kali inayotrend sasa hivi kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz kwenye social media.
 
 
Baraka aliamua kuongelea swala hili kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia amesema kuwa uteam unaoendelea baina ya wasanii ndio unaofanya wasanii kukosa tuzo nyingi na za maana na hivi ndivyo alivyoandika:
 
"Mungu saidia game ya #Tanzania tupendane na tuheshimiane(….)inasikitisha sana team team zinarudisha sana music industry yetu nyuma..tumekosa tuzo nyingi kubwa na za maana,sababu ya kukosa umoja na mshikamano wa mashabiki..tunatengeza matabaka baina ya mashabiki na mashabiki…Heee Mwenyezi MUNGU ingilia kati swala hili.. #NISAMEHE link kwa bio yangu #IamPrince #Rockstar4000 #SonyMusicAfrica."