Multichoice CEO Tim Jacobs addressing the guests during the Multichoice showcase in Mauritius

MultiChoice Africa yaand usiku wa mastaa Mauritius ambapo yaonyesha bidhaa zake mbali mbali

Ulikua ni usiku wenye vitu vingi na suprise za kutosha wa kampuni ya MultiChoice Africa ambayo ndio inamiliki product kama DStv kuonyesha bidhaa zake na kuziongelea kwa mapana zaidi mbele ya waandishi wa habari na watangazaji wa media mbalimbali za Africa.

Kwa miaka mingi nchi nyingi za Africa zimekua zikipata huduma ya TV kutoka MultiChoice na kubadilishwa kwa mfumo wa TV kuwa na mvuto na ubora zaidi kwa njia ya satellite.
 
Pamoja na waandishi na watangazaji, usiku huu ambao utaendelea kushika mpaka weekend hii hapa Mauritius, umehudhuriwa na mastaa kama Genevieve Nnaji, Rita Dominic, Desmond Elliot na Ramsey Nouah.
 
 
 
 
Kwenye sehemu ya maongezi yake kwenye usiku huu wa #OnlyTheBest C.E.O wa MultiChoice Africa Tim Jacobs alisema, "Mpango wetu ni kuhakikisha kwamba watazamaji wetu hawakosi kitu, kukua kwetu kwenye miaka 20 iliyopita ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na bado tunaendelea."
 
Aliendelea kwa kusema, "Hivyo bado mengine ambayo tulitaka yatimie hayajatimia, bado uwekezaji mkubwa unaendelea kwendana na wakati na kuhakikisha watazamaji wetu wanapata kilichobora zaidi."
 
MultiChoice inazidi kuonyesha wanahabari bidhaa zake mbalimbali kwenye wiki hii hapa Mauritius ambapo tayari wameshakutanishwa na vichwa kutoka Sony channel, TV za burudani kama MTV Base na nyingine.

Related