Rapper Rosa Ree kutoka Tanzania

Mfahamu Rosa Ree, Rapper mpya msichana anayefanya vizuri kwenye Bongofleva

Rosa Ree ni rapper msichana ambaye sio mwenyeji sana kwenye bongofleva lakini amepokelewa vizuri baada ya kutoa nyimbo yake ya kwanza One Time na sasa ana hit song nyingine inayoitwa Up In The Air ambayo pia inapata airtime ya kutosha kwenye medias Tanzania na nje.
 
Burudika na hit ya Rosa Ree kwenye Mziki Hit 10, kila Ijumaa saa 17:15 ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Akiwa chini ya usimamizi wa label ya The Industry inayomilikiwa na kundi la Navy Kenzo, Rosa Ree anakuwa kati wasichana wachache wanaofanya mziki wa rap Tanzania.
 
 
"Wapo watu wengi walikinikatisha tamaa walisema siwezi, walisema mimi msichana nawezaje kufanya mziki wa rap? Walinidharau sana sasa nataka niwaonyeshe jinsi nawaua wataelewa tu," Rosa Ree alisema.