Msanii Diamond Platnumz

Ni zaidi ya miaka mitatu sasa hivi Diamond Platnumz anaendelea kuwa staa wa kiume Tanzania alieendelea kuandikwa sana na vyombo vya habari sanasana mitandao na magazeti.

Mengi yanayoandikwa kumhusu ni maisha yake binafsi lakini pia na maisha ya muziki anaoufanya, kuanzia kwenye kuwani tuzo na mengine.
 
Mengi ya Diamond na maisha yake na pia mastaa wengine wa bongofleva, itazame Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Inawezekana wewe ni mmoja wa watu waliosoma sana au kupokea sana habari za Diamond lakini haujawahi kujua kwamba muziki anaoufanya umemuwezesha kuajiri watu wapatao 42.
 
Watu hao 42 ni kuanzia mameneja, walinzi, wafanyakazi ofisini kwake, wapiga picha na wengine ambapo anasema, "Hiyo 42 ni ukinitoa mimi na mama yangu, ukisema watu wote pamoja na mimi idadi ni 44."
 
"Ajira nyingine iko kwa dancers, mimi nina dancers wangu, Harmonize dancers wake, Raymond dancers wake na Mavoko pia atapata dancers wake, hiyo ni sehemu tu ya ajira nimeitoa," Diamond kasema.
 
Diamond Platnumz anasema siku zote atafanya kazi kwa bidii sababu muziki ndio ajira yake hakuna kingine na sasa anawania tuzo ya BET 2016, kumpigia kura nenda kwenye bio za Instagram na Twitter zake ubonyeze link utazozikuta.
 
Kwa burudani zaidi, ungana na Diamond kupitia kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.