Bongo movie star Johari

Mwigizaji Johari afafanua mengi kuhusu kilichoendelea kwenye headlines za Tanzania.

Ninae mwigizaji wa bongomovie Johari kwenye hii post na yuko tayari kutoa ufafanuzi wa kile kilichoendelea kwenye headlines za Tanzania.

Unadhani Johari atasema nini kuhusu stori za yeye kusafiri mpaka ulaya kwenda kuolewa na mzungu? Unadhani atajibu nini kuhusu stori kwamba hapatani na mwigizaji Ray?

Jiunge na waigizaji wengine kwenye bongomovie ya Offside, Jumanne 28 April saa 21:00 hapo Maisha Magic Swahili, channel 158.

Kwenye exclusive interview na dstv.com Johari amesema yeye bado hajaolewa na akiolewa hatoona noma kusema hadharani, hajawahi kuolewa na mzungu kama ilivyoripotiwa.

Kuhusu kugombana na Ray, Johari amesema sio kweli, yuko kwenye uhusiano mzuri sana na Ray ambae wanamiliki pamoja kampuni ya utengenezaji wa filamu ya RJ.

Johari ameamua pia kujikita kwenye kanda ya ziwa sasa hivi nyumbani kwao pia kwa ajili ya kutafuta vipaji vya waigizaji wapya ambapo ataanza na Shinyanga.